TIBA,UTALAAM KWENYE AFYA SASA NI 97% NCHINI
TABORA
Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mageuzi makubwa kwenye sekta ya afya kwa kuwekeza kwenye teknolojia, Elimu, wataalam, na kupeleka huduma karibu na wananchi kwa kutoa fedha zilizofanikisha ununuzi wa vifaa tiba vya uchunguzi, wizara ya afya imesema.
Kwa kipindi cha miaka mitatu, tiba, teknolojia na utaalam ambao wananchi walikuwa wakiwafuata nje ya nchi, sasa huduma hizi zinapatikana nchini kwa 97%
BAADHI YA HUDUMA AMBAZO WANANCHI SASA WANAZIPATA NCHINI NI PAMOJA NA :-
Matibabu ya ugonjwa wa Selimindu , Ugonjwa wa kibyongo
Vile vile kuna kiwanda cha kuzalisha mionzi tiba ambapo kwa Afrika ni Nchi tano pekee ( Tanzania ikiwemo) ndio zenye kiwanda kama hicho kwa sababu ya gharama kuwa kubwa na kiwanda hicho kimesaidia kuzalisha mionzi tiba ambayo ilikuwa ikitoka nje ya Nchi.
Pia Tanzania ina uwezo wa kugundua ugonjwa wa kansa kabla ya miaka mitano kutokana na uwepo wa mashine za kisasa zilizowekezwa na Dkt Samia.
