DKT SAMIA ALITIMIZA AHADI YA KUPELEKA VIFAA TIBA MISUNGWI

 

DKT SAMIA ALITIMIZA AHADI YA KUPELEKA VIFAA TIBA MISUNGWI

DKT SAMIA ALITIMIZA AHADI YA KUPELEKA VIFAA TIBA MISUNGWI

MWANZA
Ilikuwa ni Juni 14,2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Dkt Samia Suluhu Hassan katika ziara yake akizungumza na wananchi katika eneo la Kigongo alipotoa ahadi ya  kununua vifaa Vifaa tiba kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Misungwi  ili kuwezesha Wananchi kupata huduma bora za Afya Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Dkt Samia alitoa ahadi hiyo baada ya muwakilishi wa  Jimbo la Misungwi kuiomba Serikali kupeleka vifaa tiba vya kutosha katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi kusaidia wananchi kupata huduma bora za afya
Mhe Rais akijibu hoja hiyo alisema “Vifaa vya Wilaya vinakuja kila kinachopaswa kuwepo kitakuwepo pale,ninawashukuru wakandarasi kwa kazi kubwa wanayoifanya.”alisema Rais Samia.
Hatimae ahadi hiyo ya Mhe Rais Dkt Samia imetimizwa na wananchi wa wilaya ya Misungwi wanapata huduma ya afya katika hospitali hiyo