TSH BILIONI 29.1 ZATEKELEZA MIRADI MITANO MAGU

 

TSH BILIONI 29.1  ZATEKELEZA MIRADI MITANO MAGU

TSH BILIONI 29.1  ZATEKELEZA MIRADI MITANO MAGU

MWANZA
Katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2023 wilaya ya Magu imepokea kiasi cha  Shilingi  bilioni 29.1  ili kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta za utawala, afya, elimu, maji na barabara.
katika sekta ya afya, imetekeleza miradi ya Sh bilioni 2.2 ikiwa ni ujenzi wa miundombinu katika zahanati, ujenzi wa uzio katika kituo cha afya Kisesa na ununuzi wa vifaa katika vituo vya afya vya Kisesa, Kahangara, Shishani, Kabila na Lugeye.
Aidha katika sekta ya elimu halmashauri imeweza kutekeleza miradi yenye thamani ya jumla ya Sh bilioni 2.6 ikiwa ni ujenzi wa vyumba 67 vya madarasa ,
Ukamilishaji wa vyumba 15 vya madarasa , ukarabati wa vyumba vya madarasa 24 ujenzi wa nyumba 7 za walimu na ujenzi wa matundu 77 ya vyoo katika shule mbalimbali za msingi.