WANANCHI NGARA KULIPWA FIDIA SH BILIONI 26

 

WANANCHI NGARA KULIPWA FIDIA SH BILIONI 26

WANANCHI NGARA KULIPWA FIDIA SH BILIONI 26

KAGERA
KAYA 1339 katika Wilaya ya Ngara wanatarajia kulipwa kiasi cha zaidi ya Sh bilioni 26 ikiwa ni sehemu ya fidia ya ardhi iliyotolewa kupisha mradi wa uchimbaji wa Madini Mkakati ya Nikeli katika eneo la Bugarama mkoani Kagera.
Madini hayo ya Nikeli yatakayochimbwa, yatachenjuliwa na kusafishwa hapa hapa nchini Tanzania kupitia kiwanda cha kisasa kitakachojengwa Kahama mkoani Shinyanga.
Mradi huo ni wa historia katika nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara ambao utatumia teknolojia ya kisasa katika uchimbaji na uchenjuaji wa madini hayo nchini ambapo teknolojia itakayotumika ni ya kisasa ya hydro met.
KUMBUKA:-  Serikali inaandaa mkakati wa usimamizi wa madini ya kimkakati na hasa katika kusimamia uongezewaji thamani wa madini hayo hapa hapa nchini.