TSH BIL 3+ ZANUNUA MIZANI DIJITALI 1,178
LINDI
Serikali kupitia kilimo imesimamia upatikanaji wa Mizani ya Kidigiti 1,178 yenye thamani ya Shilingi 3,534,000,000.00 kupitia Vyama Vikuu vya Ushirika vya KCU (1990) Ltd, KDCU Ltd, KACU Ltd na Ushirika wa mradi wa pamoja wa korosho (KCJE) Ltd.
Mizani hiyo imesambazwa kwenye Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) vinavyojishughulisha na mazao ya kahawa, korosho, ufuta, soya, mbaazi, kakao na tumbaku katika Mikoa ya Kagera, Lindi, Mbeya, Tabora, Mtwara, Ruvuma na Pwani.
