TSH BIL 11.6 ZAJENGA GHALA 38
RUVUMA
Jumla ya Shilingi Bilioni 11.6 zilitengwa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa ghala 38 zenye uwezo wa kuhifadhi jumla ya tani 33,000 na kukamilisha ujenzi wa ghala na vihenge vyenye uwezo wa kuhifadhi jumla ya tani 165,000 katika kanda za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula nchini (National Food Reserve Agency – NFRA) za Songea Mkoani Ruvuma, Mbozi, Makambako, Dodoma na Shinyanga kupitia Mradi wa Kuongeza Uwezo wa Kuhifadhi unaotekelezwa na NFRA.
Hadi Aprili, 2024 ujenzi wa ghala 28 umefikia wastani wa 75%. Ghala hizo zenye uwezo wa kuhifadhi tani 1,000 kila moja zinajengwa katika mkoa wa Ruvuma katika Halmashauri za Songea (11), Madaba (9), Namtumbo (7) na Manispaa ya Songea (1).
Vilevile, mradi wa ujenzi wa ghala na vihenge kupitia NFRA katika kanda za Songea, Makambako, Mbozi, Dodoma na Shinyanga umefungwa na usuluhishi kwa njia ya kidiplomasia umekamilika
