HADI MACHI 2024, ABIRIA 3,202,573 WAMEHUDUMIWA (ndege)

 

HADI MACHI 2024, ABIRIA 3,202,573 WAMEHUDUMIWA (ndege)

HADI MACHI 2024, ABIRIA 3,202,573 WAMEHUDUMIWA (ndege)

TANZANIA 
Hadi kufikia Machi 2024, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ilihudumia jumla ya abiria 3,202,573 ikiwa ni sawa na ongezeko la 8.58% ikilinganishwa na abiria 2,949,508 waliohudumiwa katika kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2022/23
katika kuhakikisha ulinzi na usalama katika viwanja vya ndege nchini kwa kuzingatia miongozo ya kitaifa na kimataifa, hadi kufikia Machi 2024, TAA ilikamilisha ujenzi wa uzio wa usalama wenye urefu wa kilometa 7.2 na ufungaji wa mfumo wa taa za kuongozea ndege (AGL) katika Kiwanja cha Ndege cha Dodoma. 
Aidha, ujenzi wa uzio wa usalama pamoja na ufungaji wa mfumo wa kamera za usalama (CCTV) katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere umekamilika kwa 100%
ZINGATIA:- Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ina jukumu la kuendesha na kuendeleza Viwanja vya Ndege 58 vya Serikali vilivyopo Tanzania Bara.