JULAI 2023- MACHI 2024 STAMICO ILISAINI KANDARASI 3

 

JULAI 2023- MACHI 2024 STAMICO ILISAINI KANDARASI 3

JULAI 2023- MACHI 2024 STAMICO ILISAINI KANDARASI 3

DODOMA
Katika kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024, STAMICO ilipata kandarasi tatu (3) mpya za uchorongaji kutoka Kampuni ya Fluxing Resources ya Chemba - Dodoma yenye thamani ya shilingi milioni 650, mgodi wa Shanta Gold Mine - Singida yenye thamani ya shilingi bilioni 2.75 na Buckreef yenye thamani ya shilingi bilioni 5.01. 
STAMICO imeendelea na uzalishaji wa mkaa mbadala kutokana na makaa ya mawe unaotambulika kama Rafiki Briquettes. 
Aidha, STAMICO imeendelea na usimikaji wa mitambo miwili yenye uwezo wa kuzalisha tani 20 kwa saa katika maeneo ya Kiwira na Kisarawe kwa ajili ya kuanza uzalishaji mkubwa. 
Vilevile, shirika linaendelea na jitihada za kuongeza uzalishaji katika mradi wa mkaa mbadala wa kupikia ambapo hadi kufikia Machi 2024 Shirika limenunua mitambo mingine miwili (2) ambayo tayari imewasili nchini yenye uwezo wa kuzalisha tani 20 kwa saa na kufanya idadi ya mitambo kuwa minne (4) hadi kufikia Machi, 2024.