TSH BIL 189 ZANUNUA VIUATILIFU NA SALFA
TANZANIA
Serikali kupitia Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) kwa kushirikiana na Vyama Vikuu vya Ushirika, imetumia kiasi cha shilingi bilioni 189 kwa ajili ya ununuzi wa viuatilifu lita 2,679,520 na salfa tani 65,539.6 na kusambazwa kwa wakulima.
Pia, serikali kupitia Bodi ya Tumbaku Tanzania na Vyama Vikuu vya Ushirika imeratibu ununuzi wa viuatilifu vya zao la tumbaku Deltamethrin chupa 3,490,050, Imidacloprid pakti 1,661,929 na Flumetralin lita 166,193 zenye thamani ya Shilingi 27,630,472,800
