TSH BIL 350 KUKARABATI BARABARA
DODOMA
Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 350 kwa ajili ya ukarabati wa barabara huku pia ikiongeza bajeti ya matengenezo ya barabara kwa TARURA kutoka bilioni 21 hadi bilioni 131.
Serikali imefikia hatua hii kwakuwa inatambua umuhimu mkubwa sana wa barabara katika kuwawezesha wananchi kiuchumi na kijamii hivyo serikali itaendelea kutoa fedha na kuhakikisha barabara zinajengwa ili kurahisisha huduma hizo kote nchini.
