TSH BIL 12 MAANDALIZI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA
DODOMA
Katika mwaka 2023/24 Ofisi ya Rais – TAMISEMI iliidhinishiwa shilingi bilioni 12.00 kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwaka 2024
Hadi Machi, 2024 Ofisi ya Rais - TAMISEMI imepokea shilingi bilioni 5.6 sawa na 46.67% ya fedha iliyoidhinishwa (sh bil 12), Sehemu kubwa ya fedha ambazo hazijapokelewa zinahusika na shughuli za ununuzi ambazo taratibu zake zinaendelea.
Aidha shughuli zilizotekelezwa ni pamoja na uhakiki wa maeneo ya utawala yatakayoshiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024, kuandaa Rasimu ya Tangazo la Serikali la Maeneo ya Utawala, kuandaa rasimu ya kanuni za uchaguzi na kufanya vikao vya wadau wa ndani ya Serikali ili kupata maoni na kuyajumuisha katika rasimu ya kanuni zilizoandaliwa.
Aidha, rasimu ya kanuni hizo zitapitiwa na wadau wa nje ili kupata maoni yao kabla ya kuidhinishwa na kuanza kutumika.
kazi nyingine zilizofanyika ni pamoja na uchambuzi wa mahitaji ya vifaa vya uchaguzi (maboksi ya kupigia kura, lakiri, daftari la kuandikisha wapiga kura, nakala za kanuni, orodha ya maeneo ya utawala yatakayoshiriki uchaguzi, mihuri, wino na vidau).
Vilevile, imeandaliwa rasimu ya Mwongozo wa Elimu ya Mpiga Kura na Mwongozo wa Uchaguzi
