DKT SAMIA AKIWA PARIS
UFARANSA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan leo Mei 14,2024 ameshiriki kwenye mkutano wa kimataifa wa Nishati safi ya kupikia kwa Afrika uliofanyika katika makao makuu ya UNESCO jijini Paris Nchini Ufaransa.
Pichani ni Mhe Rais Dkt Samia akiwa na Wenyeviti Wenza, Waziri Mkuu wa Norway Mhe. Jonas Gahr Støre wa pili kutoka kulia, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina wa kwanza kulia pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kimataifa ya Nishati (IEA) Mhe. Dkt. Fatih Birol.
