SKIMU 1,987 VIJIJINI, 166 MIJINI ZA MAJI ZAHAKIKIWA

 

SKIMU 1,987 VIJIJINI, 166 MIJINI  ZA MAJI ZAHAKIKIWA

SKIMU 1,987 VIJIJINI, 166 MIJINI  ZA MAJI ZAHAKIKIWA

DODOMA
Katika kutimiza azma ya Serikali ya kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi, Wizara ya maji imeendelea kuhakiki na kufuatilia ubora wa maji katika mifumo ya usambazaji maji mijini na vijijini kwa lengo la kuhakikisha maji yanayosambazwa kwa jamii yanakidhi viwango vya kitaifa vya ubora wa maji ya kunywa.
Hadi mwezi Aprili 2023, jumla ya skimu 1,987 za maji vijijini,skimu 166 za maji mijini,  pamoja na vyanzo vya maji 245 vinavyomilikiwa na taasisi na watu binafsi vilifanyiwa uhakiki na ufuatiliaji ambapo jumla ya sampuli za maji 4,461 zimekusanywa na kuhakikiwa ubora wake. 
Matokeo ya uchunguzi yameonesha kuwa sampuli 3,190 sawa na 71.5% zilikidhi viwango