TPDC NA KAMPUNI YA MISRI ZASAINI MKATABA (LNG)
DAR ES SALAAM
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) linalomilikiwa na Serikali limesaini Mkataba wa Ubia na Kampuni ya Rosetta Energy Solutions & Africa 50 ya Misri ili kutekeleza mradi wa Mini Liquefied Natural Gas (LNG).
Utiaji saini wa mkataba huo unakwenda kupanua wigo wa usambazaji wa gesi nchini ambapo kwa sasa mikoa minne ya Mtwara, Lindi, Pwani, na Dares Salaam ndiyo imefikiwa na mtandao wa usambazaji wa gesi asilia.
Mradi wa LNG unatarajiwa kuongeza nguvu kwenye mpango wa serikali wa kuhakikisha wananchi wanatumia nishati safi ya kupikia pia kukuza usambazaji wa gesi asilia katika jumuiya ya Afrika Mashariki.
