IMF- UCHUMI WA TANZANIA KUKUA KWA 5.4%
DAR ES SALAAM.
Ripoti mpya iliyotolewa mwezi mei na shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) imesema uchumi wa Tanzania unatarajiwa kukua hadi asilimia 5.4 mwaka 2024, kutokana na kuboreshwa kwa mazingira ya biashara na kupunguza bei za bidhaa duniani.
Timu ya wafanyakazi kutoka IMF ikiongozwa na Charalambos Tsangarides, Mkuu wa Misheni ya IMF kwa Tanzania, ilifanya mikutano Dodoma na Dar es Salaam kuanzia Mei 2 hadi 17, mwaka huu, kwa ajili ya mapitio ya tatu chini ya Mpango wa Kuongeza Mikopo (ECF).
Katika mikutano hiyo ilikutanisha wizara ya fedha ya Tanzania, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), viongozi wengine wakuu, washirika wa maendeleo na wawakilishi wa sekta binafsi.
Aidha Mwezi Januari mwaka 2024 taarifa kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilikadiria ukuaji wa uchumi wa nchi kufikia asilimia 5.5 (ikiwa ni tofauti ndogo ya makadirio ya BOT na IMF) mwaka huu pia kutokana na kuboreshwa kwa mazingira ya biashara na uwekezaji wa umma katika miundombinu.
IMF imesema, BoT imesisitiza dhamira yake ya kuruhusu kubadilika zaidi kwa viwango vya ubadilishaji wa fedha ili kulipa nguvu zaidi soko la fedha za kigeni (FX) baina ya benki na kuhakikisha kiwango cha ubadilishaji kilichoamuliwa na soko.
Juhudi hizi zinatarajiwa kuendelea katika Mwaka wa Fedha 2024/25, zikiungwa mkono na sera ya ushuru na juhudi za usimamizi wa mapato kusaidia kuunda nafasi ya kifedha," inasema taarifa hiyo.
Taarifa inaongeza "serikali imejitolea kuongeza matumizi ya kijamii ya kipaumbele na kudhibiti athari za mafuriko ya hivi karibuni kwa walio hatarini zaidi."
Ajenda ya mageuzi ya kimuundo nchini inalenga kusaidia ukuaji thabiti, endelevu na shirikishi kupitia kuboresha mazingira ya biashara na kuimarisha utawala.
KUMBUKA :- Januari mwaka 2024 ripoti ya IMF ilisema Tanzania ni taifa lisilo na deni kubwa la taifa kwa nchi za Afrika.
