TANZANIA, ZAMBIA KUSHIRIKIANA MPAKANI TUNDUMA

 

TANZANIA, ZAMBIA KUSHIRIKIANA  MPAKANI TUNDUMA

TANZANIA, ZAMBIA KUSHIRIKIANA  MPAKANI TUNDUMA

SONGWE
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Mapato ya Zambia (ZRA) zimekubaliana kufanya kazi katika mpaka wa Tanzania na Zambia wa Tunduma uliopo Mkoani Songwe,kwa upande wa Tanzania.
Ushirikiano huo unalenga kuimarisha mahusiano ya kazi ili kuongeza ufanisi katika kutoa huduma kwa wasafiri kutoka nchi zote mbili.
Wakihutubia  kwenye mkutano na wanahabari, Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata, na mwenzake wa Zambia, Dingani Banda, wamesema Mamlaka hizo mbili kwa pamoja zimekubaliana kuimarisha ari ya kufanya kazi katika mpaka huo kwa sababu ni muhimu kwa manufaa ya nchi zote mbili na zitaimarisha utendakazi na uwajibikaji katika kurahisisha usafirishaji wa mizigo pamoja na kuziba mianya ya wasafirishaji wanaokwepa kodi.
Vilevile mamlaka zote mbili zimekubaliana kuweka mikakati ya pamoja ya kuboresha huduma katika mpaka wa Kasesya uliopo Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, unaolenga kupunguza msongamano wa mizigo katika mpaka maarufu wa Tunduma.
Taarifa kutoka Ofisi  ya Forodha ya TRA, inasema ukusanyaji wa mapato katika mpaka wa Tunduma kwa muda wa miezi 10 (kati ya Julai 2023 na Aprili 2024) uliongezeka hadi kufikia takribani bilioni 122.3, na kuvuka lengo lililowekwa la kukusanya shilingi bilioni 120.5  sawa na 101.5%