TANZANIA INA VIWANDA VITATU VYA VIOO
DAR ES SALAAM
Tanzania ina jumla ya viwanda vya kuzalisha bidhaa za vioo vitatu (3), Viwanda hivyo ni Kioo Ltd na Salehbhai Glass Industries Ltd ambavyo vilivyopo Mkoa wa Dar es Salaam na Sapphire Float Glass (Tanzania) Company Limited kilichopo Mkuranga Mkoa wa Pwani.
Kiwanda cha Kioo Limited huzalisha chupa za vinywaji na viwanda vilivyosalia huzalisha vioo vya majumbani (Ujenzi)
Kiwanda cha sapphire kinatumia malighafi zaidi ya 80% zinazopatikana nchini kuzalisha vioo. Malighafi hizo ni pamoja na madini aina ya dolomite, silica sand, limestone na feldspar. Kiwanda kimewekeza mtaji wa kiasi cha shilingi bilioni 800.1 na kina uwezo uliosimikwa wa kuzalisha tani 700 kwa siku sawa na tani 189,000 kwa mwaka na 60% ya vioo vinavyozalishwa na kiwanda huuzwa katika nchi za Madagascar, Burundi, Zambia, Rwanda, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) na Afrika Kusini.
KIWANDA HICHO KILIANZA UZALISHAJI MWEZI SEPTEMBA, 2023 BAADA YA KUZINDULIWA NA MHE RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN.
