DKT SAMIA AHIMIZA AMANI AFRIKA

 

DKT SAMIA AHIMIZA AMANI AFRIKA

DKT SAMIA AHIMIZA AMANI AFRIKA

DAR ES SAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amewahimiza  wajumbe wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AUPSC) kutafakari safari ya baraza hilo tangu kuanzishwa kwake, kutathmini mafanikio yake, na kujifunza kutokana na uzoefu.
Kaui hiyo ameitoa  wakati akihutubia katika Maadhimisho ya Miaka 20 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AUPSC) yaliyofanyika jijini Dar es salaam Mei 25, 2024
Akizungumza katika sherehe hizo Dkt Samia amesema   "Kwa hakika, historia ya mafanikio yetu katika harakati za ukombozi wa bara la Afrika lazima itupe motisha katika juhudi zetu za sasa za kulinda amani, kuleta maendeleo na kuhakikisha amani ya watu wetu," 
Akielezea uhai wa jambo hilo, amewahakikishia wajumbe mbalimbali waliokusanyika katika hafla hiyo kuwa Tanzania itaendelea kutoa kipaumbele katika kuhakikisha Umoja wa Afrika unafikia lengo lake.
KUMBUKA:- Baraza la Amani na Usalama (PSC) ndicho chombo cha kudumu cha AU cha kuzuia, kudhibiti na kutatua migogoro na tangu kuanzishwa kwake, hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa baraza hilo.