TANESCO KUJA NA HUDUMA KWA WATEJA (CHATBOT)

 

TANESCO KUJA NA HUDUMA KWA WATEJA (CHATBOT)

TANESCO KUJA NA HUDUMA KWA WATEJA (CHATBOT)

TANZANIA
Ili kuendelea kuimarisha utoaji wa huduma na kuongeza wigo wa mawasiliano na wateja, serikali kupitia TANESCO  katika kipindi cha Julai 2023, hadi Machi 2024 imeanzisha mfumo unaomuwezesha mteja kuhudumiwa kwa haraka zaidi bila kupiga simu kwa njia ya ujumbe wa simu (CHATBOT) ambao hadi sasa umefikia 95% ya utekelezaji wake.
Aidha Tanesco imepanua kituo cha huduma kwa wateja (Call Center) kwa kuongeza vifaa na wapokea simu kutoka mawakala 63 mpaka 100.
Kwa sasa, Shirika linakamilisha taratibu za ununuzi wa vifaa Kuanzisha mfumo utakaowawezesha wateja kupata taarifa maalumu za hali ya upatikanaji wa umeme kwa haraka kwa njia ya ujumbe wa simu kwenye simu zote janja na simu za kiswaswadu kuhusu Makatizo ya Umeme (Automatic Power Interruption Notification sytem) na hivyo kuwezesha wateja kujipanga ipasavyo na kupunguza malalamiko ya ukosefu wa umeme.