STAKABADHI GHALANI YAUZA TANI 1,656,410.28
MTWARA
Hadi Aprili, 2024 serikali/kilimo kwa kushirikiana na Bodi ya Usimamizi wa Ghala, Soko la Bidhaa Tanzania na wadau wengine imeratibu na kusimamia mauzo ya mazao ya wakulima kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala.
Jumla ya tani 1,656,410.28 za mazao zenye thamani ya Shilingi 1,977,744,859,472.50 zilikusanywa na kuuzwa kupitia mfumo rasmi wa Ushirika ikilinganishwa na tani 1,841,363.98 zilizouzwa kwa thamani ya Shilingi 1,755,121,090,813 mwaka 2022/2023.
Thamani ya mauzo imeongezeka kwa 12.7% kutoka Shilingi 1,755,121,090,813 mwaka 2022/2023 hadi Shilingi 1,977,744,859,472.50 mwaka 2023/2024
