JE WAJUA SERIKALI INAMILIKI STAMIGOLD KWA 99%

 

JE WAJUA SERIKALI INAMILIKI STAMIGOLD KWA 99%

JE WAJUA SERIKALI INAMILIKI STAMIGOLD KWA 99%

KAGERA
STAMIGOLD ni mgodi unaomilikiwa na serikali  kwa  hisa asilimia 99 kupitia STAMICO na Ofisi ya Msajili wa Hazina inamiliki hisa asilimia 1. 
Katika kipindi cha kuanzia Julai 2023 hadi Machi 2024 mgodi (stamigold) umezalisha dhahabu wakia 7,449.60 na kupata shilingi 36,579,416,773.00.
Aidha, kiasi cha shilingi 1,463,176,670.93 kimelipwa Serikalini kama mrabaha na ushuru wa huduma na shilingi 914,485,419.33 ikiwa ni ada ya usimamizi.
Pia, kwa sasa mgodi umeunganishwa kwenye Gridi ya Umeme ya Taifa ambapo imepunguza gharama za nishati kwa wastani wa kiasi cha shilingi 700,000,000.00 kwa mwezi.
Vilevile, mgodi umenunua wheel loader ambayo imesaidia kuokoa takribani kiasi cha shilingi 35,000,000.00 kwa mwezi ambazo zilikuwa zinatumika kukodisha mtambo huo