HUDUMA MPYA 16 ZA UBINGWA BOBEZI ZAANZISHWA

 

HUDUMA MPYA 16  ZA UBINGWA BOBEZI ZAANZISHWA

HUDUMA MPYA 16  ZA UBINGWA BOBEZI ZAANZISHWA

TANZANIA
Katika kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024,Serikali imeendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma  mpya 16 za kibingwa na ubingwa bobezi katika Hospitali ngazi ya Taifa, Kanda, Maalum na hospitali za Mikoa.
Huduma hizo zinajumuisha Kutenganisha mapacha walioungana kwa kutumia watalam wa ndani, Tiba hewa Mgandamizo (Hyperbaric Chamber Oxygen Therapy), Upasuaji kwa njia ya matundu madogo, Kutoa kizazi (Laparascopic Hysterectomy), Upasuaji kwa watu wenye shida ya kumeza chakula (Laparascopic Cardiomyotomy), Upasuaji rekebishi wa vipara (tissue expander), huduma ya upasuaji wa kupunguza mfuko wa chakula (Laparascopic Sleeve Gastrectomy) kwa wagonjwa wenye uzito uliopitiliza, Transcatheter Aortic Valve Implamentation (TAVI), kufungua mishipa ya miguuni iliyoziba (Endovascular Procedure – kuweka stent kwenye mishipa mikubwa ya damu iliyopasuka), Endoscopic Minimal Invasive Spine Surgery, Microscopic Minimal Invasive Spine Surgery, Spine Facet Injections for chronic Pain, Aneurysm Clipping, Intensity Modulated Radiotherapy –IMRT, 3D brachytherapy na immunotherapy. 
Vilevile serikali imewezesha Hospitali za rufaa za mikoa nane (8) kutoa huduma za kibingwa katika fani nane (8) ikilinganishwa na Hospitali za Mikoa mitano (5) kwa kipindi kama hicho mwaka 2022/23.