NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME KV 400 SINGIDA-ARUSHA – NAMANGA SASA NI 99.4%

NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME KV 400  SINGIDA-ARUSHA – NAMANGA SASA NI 99.4%

NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME KV 400  SINGIDA-ARUSHA – NAMANGA SASA NI 99.4%

SINGIDA
Serikali ya awamu ya sita inaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Singida – Arusha – Namanga
Mradi huu unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 yenye urefu wa kilomita 414 kutoka Singida hadi Namanga kupitia Babati na Arusha ambapo umekamilika kwa asilimia 99.4. 
Aidha, ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 kutoka Arusha hadi Namanga yenye urefu wa kilomita 114.3 umefikia asilimia 97.5 na kituo cha kupoza umeme cha Lemugur kimekamilika kwa 100% na kuwashwa.