KILOVITI 400 KUTOKA JNHPP ZIMEFIKISHWA CHALINZE
PWANI
Mradi wa Kusafirisha Umeme kutoka Julius Nyerere Hydro Power Plant hadi Chalinze – Kilovoti 400 na Kituo cha Kupoza Umeme, Chalinze umefikia 99.5% na njia hiyo imeanza kutumika kusafirisha umeme.
Aidha, kituo kipya cha kupoza umeme cha Chalinze cha Kilovoti 400/220/132 kimekamilika kwa asilimia 93.1 na kimeanza kutumika kuingiza umeme katika Gridi ya Taifa ambapo Kazi zilizobaki zinatarajiwa kukamilika ifikapo Juni, 2024.
