MRADI WA KUZALISHA NA KUSAFIRISHA UMEME WAENDELEA

 

MRADI WA KUZALISHA NA KUSAFIRISHA UMEME WAENDELEA

MRADI WA KUZALISHA NA KUSAFIRISHA UMEME WAENDELEA

NJOMBE
Serikali mkoani Njombe unaendelea na utekelezaji wa Mradi wa Umeme wa maji wa Rumakali ambao unahusisha ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 222 kwa kutumia maji ya Mto Rumakali mkoani Njombe na njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 64.5 kutoka kwenye mitambo hadi kituo cha kupoza umeme cha Iganjo mkoani Mbeya
Hatua zilizochukuliwa katika kutekeleza mradi huu ni pamoja na kukamilisha uthamini wa mali za wananchi watakaolipwa fidia ili kupisha eneo la mradi kwa ajili ya ujenzi ambapo taratibu za kulipa fidia zinaendelea.
Aidha, vyeti vya mazingira kutoka NEMC kwa upande wa kituo cha kuzalisha umeme na njia ya kusafirisha umeme vimetolewa na tathmini ya gharama za miundombinu wezeshi zimekamilika ambapo taratibu za kupata fedha za kutekeleza mradi na ujenzi wa miundombinu wezeshi zinaendelea