NCHI TUNAVYO VIWANDA 8 VYA KUZALISHA MAVAZI

 

NCHI TUNAVYO VIWANDA 8 VYA KUZALISHA MAVAZI

NCHI TUNAVYO VIWANDA 8 VYA KUZALISHA MAVAZI

DODOMA
Tanzania kwenye Sekta ya nguo na mavazi ina jumla ya viwanda nane (8) vinavyofanya kazi nchini katika mikoa ya Morogoro(2), Arusha (2), Mwanza, Dar es salaam(3).
Bidhaa zinazozalishwa na viwanda hivyo ni pamoja na khanga, vitenge, fulana, vyandarua, blanketi, vitambaa vya pamba (linen), nyuzi, shuka, suruali za jeans (men’s jeans) na nguo za michezo
Viwanda vya nguo vina uwezo uliosimikwa wastani wa kusokota nyuzi (spinning) tani 66,552 kwa mwaka, kufuma vitambaa (knitting) tani 7,920 kwa mwaka na uwezo wa kutengeneza nguo tofauti tofauti milioni 43 kwa mwaka. 
Kwa mwaka 2023/2024, viwanda hivyo vimezalisha nyuzi tani 46,586.4 (70%), vimefuma vitambaa tani 7,128 (90%) na kutengeneza nguo tofauti milioni 98.
Ongezeko la kutengeneza nguo limetokana na utumiaji wa vitambaa vya pamba vilivyotengenezwa na viwanda vyetu pamoja na kutumia vitambaa vya polista (polyester fabric) kutoka nje.
Aidha baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na viwanda hivyo zinauzwa nchini, zingine kwenye nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Afrika Kusini, Ulaya, Canada na Marekani kupitia Sheria ya Fursa ya Ukuaji wa Biashara Afrika (Afica Growth and Opportunity Act - AGOA) na Viwanda hivyo vimetoa ajira za moja kwa moja 15,300 na ajira zisizo za moja kwa moja 45,000