HALI YA UPATIKANAJI DAWA NCHINI UNARIDHISHA
TANZANIA
Kutokana na uwekezaji ambao Mhe Rais Dkt Samia amefanya katika sekta ya afya umechangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha hali ya upatikanaji wa dawa kwenye Zahanati ambapo ni kwa 69%, Vituo vya Afya ni 66%, Hospitali za Wilaya ni 72%, Hospitali za Rufaa za Mikoa ni 94% na Hospitali za Kanda, Maalum na Taifa ni 89%.
Aidha, katika mwaka wa fedha wa 2022/23,serikali kupitia Wizara ya afya ilifanya mapitio ya bidhaa muhimu za kipaumbele 290 kwa lengo la kuendelea kuboresha upimaji wa bidhaa hizo vituoni.
Kufuatia mapitio hayo, kwa sasa Zahanati zinapimwa kwa aina 100 ya bidhaa za afya, Vituo vya Afya aina 178 Hospitali za Halmashauri aina 203, Hospitali za Rufaa za Mikoa aina 245 na Hospitali za Kanda na Taifa ni aina 290.
Upimaji huo pia umezingatia mahitaji ya Hospitali Maalum kama JKCI, ORCI, Mirembe na Kibong`oto.
