NCHI INA VITANDA 145,374 VYA KULAZA WAGONJWA
TANZANIA
Serikali ya awamu ya sita kupitia Wizara ya afya imeendelea kuboresha mazingira ya kutolea huduma za afya kwa wananchi katika vituo vya kutolea huduma kwa kuongeza vitanda kutoka 126,036 vilivyokuwepo mwaka 2022/23 hadi kufikia vitanda 145,374 Machi 2024 ikiwa ni sawa na ongezeko la 15.3%
Aidha, kati ya vitanda hivyo, vitanda 47,177 vipo katika ngazi ya Hospitali, vitanda 34,328 vipo katika Vituo vya Afya, vitanda 42,390 vipo katika Zahanati na vitanda 21,539 vinapatikana katika kliniki na vituo vinginevyo.
