MBEGU BORA SASA NI TANI ELFU 68+
DODOMA
Hadi Aprili, 2024 upatikanaji wa mbegu bora umefikia tani 68,473.67 ikilinganishwa
na tani 64,152.11 mwaka 2022/2023.
Upatikanaji huo ni sawa na 54% ya mahitaji ya tani 127,650 kwa mwaka. Aidha, uzalishaji wa mbegu bora ndani ya nchi umefikia tani 49,414 sawa na ongezeko la 11.4% ikilinganishwa na tani 44,344.4 zilizozalishwa mwaka2022/2023.
Uzalishaji wa mbegu bora ndani ya nchi umechangiwa na ASA, TARI na Sekta binafsi.
