MIAKA MITATU SEKTA YA UCHUKUZI YAKUA KWA 50%
DODOMA
Katika kipindi cha miaka mitatu, mchango wa sekta ya uchukuzi kwa fedha za kigeni umeongezeka kutoka Dola za Marekani bilioni 1.6 mwaka 2022 hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 2.4 mwaka 2024, sawa na ongezeko la 50% katika kipindi hicho
Sekta ya Uchukuzi imeendelea kutoa mchango wa ukuaji wa Uchumi kwa Taifa kwa kuwa ni sekta wezeshi katika kuchagiza ukuaji wa sekta nyingine za uzalishaji zikiwemo sekta za kilimo, madini, utalii, viwanda na biashara pia ni ya tatu (3) kwa kuchangia fedha za kigeni kupitia mauzo ya huduma (Trade in Services).
