FILAMU YA AMAZING TANZANIA YAZINDULIWA

 

FILAMU YA AMAZING TANZANIA YAZINDULIWA

FILAMU YA AMAZING TANZANIA YAZINDULIWA

CHINA
FILAMU mpya ya kuitangaza Tanzania iitwayo ‘Amazing Tanzania’iliyomshirikisha Rais Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  Dkt Hussein Ali imezinduliwa rasmi  tarehe 15, Mei 2024 katika jiji la  Beijing nchini China.
Filamu hiyo pia imechezwa na Mchezaji Filamu kutoka nchini China ajulikanaye kwa jina la Jin Dong na imefanyika katika maeneo ya Zanzibar na  hifadhi ya Arusha ambako kuna maeneo yamefanywa na Mhe  Rais  Dkt Samia na mengine Dk Mwinyi.
Filamu ya Amazing Tanzania inakuwa filamu ya pili kwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan baada ya kucheza  Royal Tour  ambayo alikuwa muhusika  mkuu na ilizinduliwa jijini New York, Marekani na baadae hapa nchini ilizinduliwa Arusha Aprili 28 ikifuatia Zanzibar Mei 7 na kuhitimishwa kitaifa Dar es Salaam, Mei 8, 2022  na Rais Samia alianza kurekodi filamu hiyo Agosti 29, 2021 kwa lengo la kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia vivutio vya utalii.