ATCL INATOA HUDUMA VITUO 24 NDANI & NJE
DAR ES SALAAM.
Katika kuendelea kuongeza wigo wa huduma zake, ATCL imeendelea kutoa huduma ya usafiri wa anga katika vituo 11 vya nje ya nchi (Bujumbura, Dubai, Entebbe, Hahaya, Guangzhou, Harare, Lubumbashi, Lusaka, Mumbai, Nairobi na Ndola) huku ikitoa huduma katika vituo 13 vya ndani katika mikoa ya Arusha, Bukoba, Dar es Salaam, Dodoma, Geita, Kilimanjaro, Kigoma, Songwe, Mpanda, Mwanza, Songea, Tabora na Zanzibar na kufanya jumla ya vituo vyote kufikia 24.
Aidha hadi kufikia Machi, 2024, ATCL ilisafirisha abiria 850,660 ikilinganishwa na abiria 826,594 waliosafirishwa katika kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2022/23 sawa na ongezeko la 2.91%.
Vilevile, ATCL imesafirisha jumla ya tani 5,034.2 za mizigo ndani na nje ya nchi ikilinganishwa na tani 2,680.9 katika kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2022/23 sawa na ongezeko la 87.78%.
ZINGATIA:- Ongezeko hilo limetokana na kuanza kufanya kazi kwa ndege ya mizigo aina ya Boeing 767-300F yenye uwezo wa kubeba tani 54.
