DKT SAMIA KUONGOZANA NA WASANII KWENYE ZIARA
DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amesema anafikiria kuanza kuongozana na wasanii pindi anapokuwa kwenye ziara za nje ya nchi.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa Albam ya Rajab Abdul (Harmonize) uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam Mei 25, Dkt Samia amesema “tunapokwenda kwenye ziara nafuatana na jopo la wafanyabiashara, nataka sasa niwe nachukua wasanii,kila tunapokwenda kukiwa na matamasha ya utamaduni nitabeba wasanii,Amesema Dkt Samia.
Aidha Dkt Samia amesisitiza kwamba akiwa kwenye ziara atatafuta nafasi za mafunzo kwa wasanii hasa waigizaji na ufuatiiaji wa suala hilo atauanza hivi punde atakapokuwa ziarani nchini Korea Kaskazini.
