DKT SAMIA AWATAKA WASANII KUWEKEZA
DAR ES SAAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka wasanii wa muziki na filamu kuwekeza kutokana na kipato wanachokiingiza wakati wa sasa wanapofanya shughui za sanaa.
Mhe Samia ametoa wito huo Mei 25, 2024 wakati akishiriki uzinduzi wa albam ya msanii Rajab Abdul (Harmonize) uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Dkt Samia amesema “wekezeni katika sekta mbalimbali,tutafika pahali sauti zinagoma, kuwe kuna kitu kinakusaidia,wanaofanya filamu hivyohivyo, wekezeni ili maisha kule mbele yaende kuwa mazuri”
