UWEKEZAJI KIDIJITI WAWALETA WA- SUDAN KUSINI & BURUNDI NCHINI

 

UWEKEZAJI KIDIJITI WAWALETA WA- SUDAN KUSINI & BURUNDI NCHINI

UWEKEZAJI KIDIJITI WAWALETA WA- SUDAN KUSINI & BURUNDI NCHINI

DAR ES SALAAM.
Wajumbe kutoka Sudan Kusini na Burundi wapo nchini kujifunza namna Tanzania ilivyofanikiwa kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara kupitia mfumo wa usajili wa kidijitali.
Katika ziara yao wajumbe hao wamekutana na maofisa wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ambao waliwaeleza kuhusu Mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandao na majukwaa mengine.
Mkuu wa Idara ya Usajili wa Biashara Burundi Shirika la Maendeleo la Burundi, Alida Mugisha amesema wamekuwa wakitumia mfumo uliotengenezwa na BRELA tangu 2022 lakini bado wanakabiliwa na changamoto.
"Tumekuja tena kujifunza jinsi ya kukabiliana na changamoto zinazojitokeza wakati wa utumiaji wa mfumo ili kuimarisha urasimishaji wa biashara," amesema Mugisha
Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Makampuni ya Biashara kutoka Wizara ya Sheria, Jamhuri ya Sudan Kusini, Bw Madol Anyuat amesema ziara yao itawasaidia kujifunza, kuboresha mifumo yao na kuvutia urasimishaji zaidi wa biashara.