TSH BIL 60.1 ZA SUMBAWANGA AIRPORT ZAANZA KAZI
RUKWA
Kiasi cha shilingi bilioni 60.1 kilichotolewa na serikali ya awamu ya sita kwa ajili ya uboreshaji na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Sumbawanga kimeanza kufanyiwa kazi kwani sasa ujenzi wa kiwanja hicho umefikia 9.0% ya uteklezaji huku ukitarajiwa kukamilika Machi 2025 na kufungua kwa kasi uchumi wa ukanda wa Nyanda za juu kusini na kuimarika huduma ya usafiri wa anga katika eneo hilo.
Hadi sasa, mkandarasi wa mradi huo Bi Beijing Construction Engineering Group Co Ltd (BCEG) ameshalipwa malipo ya awali ya zaidi ya shilingi bilioni 8.0 na mradi huu utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuhudumia Bombardier - 8 Q 400 na ATR 72 , utakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria 150,000 kila mwaka pamoja na shughuli za utalii na usafirishaji wa bidhaa na huduma, pia utafanya kazi mchana na usiku.
Aidha mradi wa ukarabati na upanuzi huo unahusisha njia ya kuruka na kutua ndege itakayoruhusu ndege kuruka mita 1.750 na upana wa mita 30 kwa kiwango cha lami, kukamilika kwake pia kutasaidia ndege kufanya upakiaji na upakuaji wa mizigo.