BAJETI YA UVUVI YAPAA KWA MARA NNE
DAR ES SALAAM.
Serikali ya awamu ya sita imeleta mageuzi kwenye izara ya mifugo na uvuvi wa kupandisha bajeti kutoka shilingi bilioni 66.5 mwaka 2021/2022 hadi shilingi bilioni 295.9 kwa mwaka 2023/2024 ikiwa ni ongezeko karibia mara nne ya bajeti ya mwanzo.
Ongezeko la bajeti hiyo imeisaidia wizara hiyo kupiga hatua kwenye utendaji wa kazi ambapo kwa sasa Tanzania imefanikiwa kupeleka nyama nchi kama za Dubai na Saudia kitu ambacho miaka ya nyuma hakikuwahi kuwepo.
Kupitia maboresho yanayofanyika kupitia wizara ya uvuvi na mifugo, ujenzi wa Bandari ya Uvuvi Lindi umefikia 52% ambao ujenzi wake hadi kukamilika utatumia gharama ya Sh bilioni 289 ikiwa na lengo la kufungua uchumi wa Buluu.
Aidha mradi wa Building Better Tomorrow (BBT) kwa upande wa Mifugo na Uvuvi imefanya kazi kwenye vituo nane na sasa vinaenda kuwa vituo 13 ambapo walinunuliwa ng’ombe 2,348 na waligawanywa kwenye vituo nane ikiwemo Tanga, Mwanza na Kagera na tayari faida ya zaidi ya Sh milioni 100 imepatikana kwenye mradi huo wa BBT.
Halikadhalika maeneo 51 ya minada 51 yamejengwa yenye thamani ya Sh bilioni 17.5 na ng’ombe zaidi Sh milioni 12 imeuzwa kwenye minada hiyo, na tayari wizara imepata ithibati ya mbegu za malisho ambazo wafugaji wataenda kununua kwa ajili ya kipindi cha kiangazi ili wafugaji wasikose malisho.