TANZANI, MISRI KUKARABATI BARABARA UNGANISHI
DAR ES SALAAM,
Tanzania na Misri zimekubaliana kushirikiana katika kukarabati sehemu ya Barabara Kuu ya Cairo-Cape Town inayovuka Tanzania, kwa lengo la kufungua na kurahisisha usafiri katika mataifa hayo mawili.
Kupitia mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar es salaam siku ya jumanne (Februari 20) kati ya wizara ya ujenzi ya Tanzania na Waziri wa Uchukuzi wa Misri, Luteni Jenerali Kamel Al Wazir taarifa inasema njia hiyo inaunganisha nchi za Kaskazini na Kusini mwa Afrika kupitia Afrika Mashariki na ina urefu wa kilomita 10,228, kati ya hizo kilomita 1,600, kwa mujibu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), ziko Tanzania.
Mikoa ya Tanzania iliyounganishwa na njia ndefu zaidi barani Afrika ni pamoja na Songwe, Mbeya, Iringa, Dodoma, Manyara, na Arusha.
Hivyo kufuatia hali hiyo, Tanzania ni lango la kimataifa kwa baadhi ya nchi jirani zisizo na bandari kama Burundi, Rwanda, Uganda, DR Congo, Zambia na Malawi, ambapo kupitia mtandao wetu mpana wa barabara wanapata soko la kimataifa.
Aidha kukarabati kwa barabara hiyo na Kufikiwa kwa sehemu hiyo kwa viwango vinavyohitajika vya kimataifa, kutachochea ukuaji wa uchumi wa nchi.