DKT SAMIA AWASIHI WATANZANIA KUDUMISHA AMANI,UZALENDO
DODOMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania kuendelea kudumisha amani,umoja, uzalendo na mshikamano wa Taifa ili kuendelea kuwaenzi waasisi wa Muungano kwa vitendo.
Mhe Dkt Samia ametoa rai hiyo leo April 24 katika viwanja vya ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma alipokuwa akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa vitabu viwili vya Muungano kikiwemo Kitabu cha Miaka 60 ya Historia ya Ofisi ya Makamu wa Rais.
Dkt Samia amesema “Naomba niwasihi Watanzania wote kuendelea kudumisha amani,umoja na mshikamo wa Taifa letu, tuendelee kufanya kazi wa bidii,na kuendelea kudumisha uzalendo kwa kuwaenzi kwa vitendo waasisi wetu”
Aidha kupitia hafla hiyo Mhe Rais ameagiza kuandaliwa chapisho lililotafsiriwa kwa Kiswahili kutoka kwenye moja ya vitabu vilivyozinduliwa leo kuhusu miaka 60 ya Muungano (Sixty Years Of The United Reblic Of Tanzania) kiwekwe kwenye lugha ya Kiswahili ili kuwafikia watanzania walio wengi zaidi.
“Tukitafsiri kitabu hiki kwa Kiswahili, na mimi nitakuwa mdhamini wa hiyo kazi” Ameongeza Rais Samia.