UJENZI WA BARABARA SANZATE-NATA NI 45%

 

UJENZI WA BARABARA SANZATE-NATA  NI 45%

UJENZI WA BARABARA SANZATE-NATA  NI 45% 

MARA
Ujenzi wa barabara ya Sanzate – Nata iliyopo Wilaya ya Serengeti mkoani Mara kwa kiwango cha lami umefikia asilimia 45 na inatarajiwa kukamilika ifikapo Januari, 2025.
Mpango wa serikali ni kuijenga barabara yote kutoka Mugumu – Natta – Sanzate hadi makutano kwa kiwango cha lami, ili kurahisisha mawasiliano kwa wananchi wa Serengeti na maeneo jirani.
Aidha Barabara ya Kilindoni – Rasi Mkumbi Wilaya ya Mafia mkoani Pwani, ipo kwenye mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na itajengwa kwa kiwango cha lami.