DKT SAMIA ANG’ARISHA SEKTA YA BENKI

 

DKT SAMIA ANG’ARISHA SEKTA YA BENKI

DKT SAMIA ANG’ARISHA SEKTA YA BENKI

DAR ES SALAAM
Ndani ya kiindi cha uongozi wa Dkt Samia Suluhu Hassana, sekta ya benki imekua kwa kasi katika miaka mitatu iliyopita, kutokana na mazingira mazuri ya kiuchumi yanayoambatana na kushuka kwa mfumuko wa bei.
Sekta hiyo mwaka jana ilikua kwa 16%, na kufuatiwa na sekta ya madini iliyokua kwa  10.2% kutokana na kuongezeka kwa kasi ya uchimbaji 
Sekta nyingine zilikuwa umeme (10%), sanaa na burudani (10%), malazi na chakula (8.9%) na habari na mawasiliano (7.9%).
Taarifa kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inasema mafanikio ya sekta ya benki yamechangia kwa kiasi kikubwa mchango wake katika Pato la Taifa kufuatia utekelezaji sahihi wa sera ya fedha inayorahisisha michakato mbalimbali mabayo serikali ya awamu ya sita imefanikisha.
Vile vile, sekta hiyo imeshuhudia ongezeko la huduma mpya za kifedha na mabadiliko katika mifumo ya utoaji huduma, ikisaidiwa na ubunifu na mabadiliko ya teknolojia. Hadi sasa shughuli mbalimbali kama vile uhamisho wa pesa, malipo ya ankara na kodi, pamoja na huduma nyingine zinafanywa kwa haraka kwa mifumo ya dijitali.
Sanjari na hayo kiwango cha ushirikishwaji wa fedha nchini kimeongezeka hadi 76% mwaka 2023 kutoka 65% mwaka 2017.
ZINGATIA:- Lengo la Mpango wa Maendeleo wa Taifa ni kuendelea kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi ambao ni shirikishi