MIRADI YA BARABARA INAYOTEKELEZWA ARUSHA
Serikali mkoani Arusha inatekeleza miradi mbalimbali ya mtandao wa barabara kwa kiwango cha lami.
Baadhi ya miradi hiyo ni pamoja na Mtandao wa barabara yenye urefu wa kilomita 9.3 wa njia nne kwa kiwango cha lami ambayo itaanza kutandazwa kutoka eneo la Triple A’ itakayounganisha Barabara ya Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) kuelekea mzunguko mkuu wa Kisongo kupitia barabara kuu ya Dodoma.
Pamoja na ujenzi wa barabara hiyo Serikali mkoani Arusha inatekeleza miradi mikubwa ya barabara itayounganisha Arusha na mikoa mingine ikiwemo urefu wa kilomita 453 itakayounganisha jiji la Arusha na wilaya ya Kongwa Dodoma kupitia wilaya za Simanjiro na Kiteto.
Barabara nyingine ni yenye urefu wa kilomita 339 itakayounganisha miji ya wilaya ya karatu Mkoani Arusha na wilaya za Mbulu na Hydom mkoani Manyara ambayo itafikia mto sibiti,Singida na Lalago hadi Maswa Mkoani Simiyu.