UJENZI SOKO LA KARIAKOO WAFIKIA 93%
DAR ES SALAAM
Ujenzi wa soko jipya la kariakoo lenye ghorofa sita za juu na ghorofa mbili za chini na ukarabati wa jengo kuu la soko la Kariakoo umefikia 93% ya utekelezaji huku Mkandarasi ESTIM Construction Ltd ya Dar es Salaam anaetekeleza mradi huo akilipwa shilingi 17.24 kati ya shilingi bilioni 28.03 gharama halisi za mradio huo hadi kukamilika kwake.
Mradi huo ulianza kutekelezwa Januari, 2022 na unatarajiwa kuanza biashara mwanzoni mwa mwaka 2024/25 huku mtaalamu mshauri akiwa ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
