BAJETI YA BARABARA DODOMA YAFIKIA TSH BIL 34.2
DODOMA
Serikali ya awamu ya sita imeongeza bajeti ya ujenzi, matengenezo na ukarabati wa miundombinu ya barabara kwa mkoa wa Dodoma kutoka shilingi bilionin12.7 mwaka 2021 hadi shilingi bilioni 34.2 mwaa 2023/2024.
Kufuatia ongezeko hilo la bajeti, miundombinu ndani ya Mkoa wa Dodoma imeendelea kuimarika ambapo imefanikisha kupunguza wastani wa 60% ya barabara zilizokuwa na hali mbaya mwaka 2020/2021 hadi kufikia 3% mwaka 2023/2024.
Mafanikio mengine katika miaka mitatu ya Mhe Rais Dkt Samia ni kuongezeka kwa mtandao wa barabara za lami kutoka Km 171.29 hadi Km 309.71,barabara za changarawe kutoka Km 1258.65 hadi Km. 1827.5 pamoja na ufunguzi wa barabara mpya jumla ya Km 544.60
Aidha jumla ya madaraja 19, maboksi kalavati 45, mifereji ya maji ya mvua yenye urefu wa mita 73,822.24 yamejengwa na jumla ya taa za barabarani 470 zimewekwa.
Mkoa wa Dodoma una mtandao wa barabara wenye jumla ya urefu wa Km 7,540.9.
