TZ KUWA MWENYEJI MKUTANO WA UCHUMI WA BULUU

 

TZ KUWA MWENYEJI MKUTANO WA UCHUMI WA BULUU

TZ KUWA MWENYEJI MKUTANO WA UCHUMI WA BULUU

DAR ES SALAAM
Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji kwenye mkutano wa tatu wa uchumi wa buluu (BEC) unaotarajiwa kufanyika Jijini Dar es salaam kuanzia Julai 11 hadi 13, mwaka 2024 huku nchi za Korea Kusini, Ghana, na Sweden zikiwa ni miongoni mwa nchi zinazotarajiwa kushiriki katika Mkutano huo.
Mkutano huo umeandaliwa kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Mkoa wa Bahari cha Ghana ili kuendeleza uchumi wa bluu barani Afrika huku  Mada za mkutano huo ikizingatia maeneo makuu manne.
Ari ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kufungua milango kupitia diplomasia ya uchumi ndio imekuwa nguzo muhimu ya kufanikisha mkutano huo kufanyika nchini Tanzania.