KODI TUNAZIHITAJI, LAKINI KODI ZA DHULUMA HAPANA!!-DKT SAMIA
DAR ES SALAAM
Kupitia baraza la Idd-El-Fitri lililofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNCC) Dar es Salaam tarehe 10 Aprili, 2024 Mhe Rais Dkt Samia amewahimiza mamlaka ya mapato Tanzania kuendelea kukusanya kodi huku akisistiza ukusanyaji wa kodi za halali.
Kupitia baraza hilo Dkt Samia amesema mnamo tarehe 6,mwezi wa April Mwaka 2021 baada ya kumuapisha kamishna mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania alimsisitiza kuhusu ukusanyaji wa kodi za halali
“Nilimwambia kwa msisitizo kwamba nenda kakusanye kodi, kodi tunazihitaji,lakini kodi za dhuluma Hapana”Amesema Dkt Samia
Aidha ameongeza “Nilisema hivyo kwa kutambua kwamba serikali inahitaji mapato yatokanayo na kodi ili iweze kutimiza wajibu wake kuhakikisha wananchi wanapata huduma ikiwemo za kijamii,nilisisitiza haki kwenye ukusanyaji wa kodi, nikiamini kwamba Penye dhuluma Baraka za Mungu haziingii”
Mhe Rais amehitimisha kwa kusema kwamba “napenda kusisitiza msimamo wangu wa kutokubaliana na kodi za dhuluma”Amesisitiza Dkt Samia.