WATUMISHI WAPYA 33,212 KUAJIRIWA

 

WATUMISHI WAPYA 33,212  KUAJIRIWA

WATUMISHI WAPYA 33,212  KUAJIRIWA

TANZANIA

Mhe. Rais  Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa kibali cha kuajiriwa watumishi wapya 33,212 katika mwaka huu wa fedha huku jumla kuu ya watumishi wanaotarajiriwa  kuajiriwa katika mwaka wa fedha  2025/26 ikitarajiwa kufikia 41,500 

Katika kibali cha ajira 33, 212 kilichotolewa na Mhe.Rais Dkt Samia wamo walimu 10,000 na wataajiriwa bila kufanyiwa usaili na serikali itawachukua kwenye kanzidata yake.

 
Aidha,kuanzia Julai mwaka huu mwongozo wa ajira za kujitolea utaanza rasmi kufanya kazi na watakaojitolea watapatiwa stahiki zao ikiwemo fedha za kujikimu.

MUHIMU:- Katika utumishi wa umma hakuna msamiati wa ajira za muda na ndio maana imekuja msamiati wa ajira za kujitolea, hivyo itaweka mfumo wa kupata stahiki za kujikimu na umewekewa muongozo ili wanaojitolea watendewe haki