TUNAENDELEZA MIJADALA YA KITAIFA-DKT SAMIA

 

TUNAENDELEZA MIJADALA YA KITAIFA-DKT SAMIA

TUNAENDELEZA MIJADALA YA KITAIFA-DKT SAMIA

ARUSHA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema Taifa bado linaendelea kuuenzi mchango wa aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania hayati Edward Moringe Sokoine kwa kuruhusu mijadala mbalimbali ya kitaifa pale inapotakiwa kufanyika hivyo.
Dkt Samia ametoa kauli hiyo (leo) April 12, 2024 akihutubia kwenye Misa Maalum ya miaka 40 ya Kumbukumbu ya kifo cha Hayati Edward Moringe Sokoine, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Nyumbani kwa Hayati Sokoine Monduli Juu, Mkoani Arusha.
Mhe. Rais Samia amesema  Hayati Sokoine alikuwa ni mpenda maendeleo kwa nyakati mbalimbali, alisisitiza kwamba kazi mojawapo kubwa ya wanazuoni ni kuongoza mijadala kuhusu namna ambavyo nchi inavyoweza kujieleta maendeleo,aidha aliwataka kuhakikisha mawazo yao ya kimaendeleo yanawafikia watunga sera,vyama vya siasa na watendaji wa serikali “ na haya kwa bahati nzuri tunayaendeleza,kila linapotokea jambo kubwa la kitaifa mijadala inafanyika kwenye redio na maeneo mbalimbali”  Amesema Dkt Samia
Hayati Sokoine alizaliwa Agosti 1, 1938 katika kijiji cha Enguik wilayani Monduli mkoani Arusha na kufariki mwaka 1984.