NAMKUMBUKA SOKOINE KUHUSU ELIMU,ASEMA RAIS SAMIA
ARUSHA
Mhe Rais Dkt Samia amesema anamkumbuka hayati Edward Moringe Sokoine kuhusu inayohitajika kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
Dkt Samia ametoa kauli hiyo tarehe 12 April,2024 wakati akihutubia kwenye Misa Maalum ya miaka 40 ya Kumbukumbu ya kifo cha Hayati Edward Moringe Sokoine, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Nyumbani kwa Hayati Sokoine Monduli Juu, Mkoani Arusha na kusema Hayati Moring Sokoine.
Akimnukuu amesema “elimu inayohitajika vijijini kwanza kabisa ni kuimarisha na kuinua ustaarab ili watu wasiridhike na maisha duni waliyonayo” huku akiongeza kwamba elimu aina ya pili ni ufundi, elimu ya kuelewa mazingira ya kijamii ili watu walelewe nafasi zao katika jamii wanazoishi.
Mhe Rais ameongeza serikali imeyafanyia kazi maono ya hayati Sokoine kwani kuanzia januari mwaka huu (2024) nchi imeanza kutekeleza sera ya elimu iliyoboreshwa inayojielekeza katika kuleta mageuzi makubwa vijijini kupitia elimu,huku maboresho yaliyofanyika ikiwa ni pamoja na kuweka msisitizo kwenye elimu ya ujuzi ili wanafunzi wakihitimu wawe na uwezo zaidi wa kuchangia katika jamii zao.