TSH BIL 863.78 ZA MADUHULI NA MAPATO ZAKUSANYWA

 

TSH  BIL 863.78 ZA MADUHULI NA MAPATO ZAKUSANYWA

TSH  BIL 863.78 ZA MADUHULI NA MAPATO ZAKUSANYWA

DODOMA
Katika mwaka 2023/24, taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI, mikoa na mamlaka za serikali za mitaa hadi Machi, 2024 zimekusanya kiasi cha shilingi bilioni 863.78 sawa na asilimia 72.02 ya lengo lililotakiwa kukusanywa za maduhuli na mapato ya ndani ya shilingi trilioni 1.19 
Kati ya fedha hizo shilingi bilioni 848.14 ni mapato ya ndani ya mamlaka za serikali za mitaa, shilingi bilioni 15.44 ni mapato ya ndani ya taasisi name shilingi milioni 193.79 ni maduhuli ya mikoa.
Makusanyo hayo yametokana na ada za wanachuo, tozo, ukusanyaji wa madeni, mauzo ya bidhaa mbalimbali na ushuru unaotozwa na mamlaka za serikali za mitaa kulingana na Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sura ya 290.